"'Wasanii kununua airtime na kutoa pesa nyimbo fulani zisipigwe ni msiba mkubwa' "Kala Pina"

Kiongozi wa kundi la Kikosi cha mizinga, Kala Pina ameeleza kuwa kuna mabadiliko makubwa sana kwenye kiwanda cha muziki Tanzania kwa kulinganisha na hali ilivyokuwa zamani na kuonesha kuchukizwa na kile anachodai kuwa wasanii au wadau wa muziki kulipia nyimbo zao kupigwa redioni.

Kala Pina ameimbia The Jump Off ya 100.5 Times Fm wakati anauzungumzia wimbo wake mpya ‘Hip Hop is Alive’, kuwa hivi sasa kuna watu ambao wanatoa pesa kwa ajili ya kuzima baadhi ya nyimbo zisipigwe redioni na kwamba hali hii ni msiba mkubwa.




“Wasanii wanatoa pesa kununua airtime halafu wanatoa pesa kukandamiza ngoma za watu wengine zisipigwe kwenye redio zetu. Kwa hiyo huo ni msiba mkubwa naweza kusema umepeleka muziki wetu kuonekana unakwenda lakini mimi naona umestack.” Amesema Kala Pina.

“Sasa hivi mtaa zinasikilizwa ngoma za ki-Nigeria, kwenye maharusi zinasikilizwa ngoma za ki-Nigeria na ukikaa baa zinasikika ngoma za Ki-Nigeria wakati muziki wetu upo. Hii inatokana na vijana ambao wanapata nafasi wananunua hizi airtime hawapigi nyimbo ambazo zinapatikana.” Ameongeza Kala Pina.

Alieleza pia lengo la kutoa wimbo huo ukiwa ni wimbo wake wa kwanza kwa mwaka huu:

“Nimeamua kutoa hii ngoma ‘Hip Hop is Alive’ kwamba Hip Hop inaishi na wenyewe hip hop tupo na nimeamua kutoa hii ngoma kurudisha attention ya watanzania kuweza kusikiliza ngoma zetu. Ni ngoma ya kimataifa na unaweza kuipiga katika nchi yoyote na ikakalisha mtu yeyote. Na baada ya kuona vijana wanadiss hip hop sijui ma-MC mnaimba nini mara bangi mara matusi sijui nini. Kwa hiyo tunajaribu kuwaonesha kwamba sisi watu wa hip hop tukiamua kutoa ngoma kali tunaweza kutoa ngoma kali kushinda wao. Ndio nia na madhuni ya hii ‘Hip Hop is Alive’.”





Credit:TimesFm
Previous Post Next Post