Victoria Kimani aeleza atakavyomtambua mwanaume anayempenda kwa dhati, adai itamchukua wiki mbili tu

Mwanamuzi wa Kenya, Victoria Kimani ameiambia tovuti ya Times Fm kupitia segment ya ‘Times Q&A’ kuwa itamchukua wiki mbili tu kumfahamu mwanaume ambaye anampenda kwa dhati katikati ya wengi ambao wanaigiza kuwa wanapenda.

“Unasoma ishara, kila wakati kuna ishara, nadhani utakuwa unafahamu kama mtu anakupenda kweli kwa sababu vitendo vinaongea zaidi ya maneno.” Amesema Victoria Kimani.


Hata hivyo member huyo wa label ya Chocolate City anatambua kuwa kuna waigizaji wazuri katika kuonesha vitendo ili kumchanganya mrembo kama yeye ahisi anapendwa kweli. Hapo maombi ndiyo ngao yake pekee.

“Lakini wakati mwingine mtu anaweza kuonesha matendo lakini hawakupendi kwa hiyo inakuwa kama mchezo. Kwa hiyo inabidi kuomba, naamini katika maombi, naomba mara kwa mara ‘Mungu anioneshe kama kweli mtu huyu ananipenda au hapana’. Kwa kawaida ntafahamu ndani ya wiki mbili.”

Mrembo huyo ameeleza sifa za mwanaume ambaye angependa kuwa naye katika mahusiano ya mapenzi kama boyfriend na kisha mume wake wa ndoa.



“Tunaweza kuanza na ‘boyfriend material’ kwanza kabla ya kwenda kwa mume wa ndoa? Sijui…nataka mtu yeyote ninaem-date kuonesha anajivunia kuwa na mimi, anioneshe mapenzi, anipeleke sehemu zote, nataka awe ni mtu mwenye hisia kwa Mungu, awe mchapakazi na mbunifu kwenye mambo yake anayofanya. Mtu ambaye sio ana ratiba moja anayoifuata kila siku. Nataka mtu anaebadilisha ratiba huenda siku moja ananiambia twende tukapande mlima au twende tukaogelee baharini.

“Nataka kuwa na furaha na kupata starehe, nadhani watu wanapoanza kuzeeka ndipo wanapoanza kushangweka. Unapozidi kupata furaha ndivyo unavyozidi kubaki kijana milele. Kwa hiyo nataka yeyote ntakayekuwa nae nataka awe anapenda kushangweka, hata kama tukifikisha miaka 50 au 60.”


Credit:TimesNews

Previous Post Next Post