Mashahiri ya Wimbo wa Lady Jay Dee - Historia.

Soma mashahiri yaliyotumika katika wimbo mpya wa lady jay Dee Unaoitwa Historia, amabapo wimbo huo umefanyika katika studi za Combination Sound Chini ya Producer Man Water

Wimbo Umeandikwa na : JUDITH WAMBURA (LADY JAY DEE)
Producer: MAN WATER
Studio: COMBINATION SOUND
CHORUS:
Unakubalije uwe historia,
Kabla siku yako haijafika
Iweje leo uwe historia,
Kabla siku yako haijafika.
VERSE 1:
Muda huo muda ulikuwepo
Muda huo uliopewa
Hela nazo zilikuwepo
Hela ulizo barikiwa
Maisha mazuri, nyumba nzuri
Gari zuri, na nini na nini
Muda huo uliuchezea
Pesa nazo ulizichezea
Kabla hata ya uzee haujaja
Wamesha sema aaah!! alikuwaga
CHORUS:
Unakubalije uwe historia
Kabla siku yako haijafika
Iweje leo uwe historia
Kabla siku yako haija fika
VERSE 2:
Tena hata, hata wenzio
Ulo kuwa nao jana
Hata nao wanakusema, mbali na kukucheka
Umegeuka story, umekuwa mfano
Umegeuka tukio, sio kivutio
Muda huo uliuchezea
Pesa hizo ulizichezea
Kabla hata ya kifo chako
Walisha sema aaah! alikuwaga
Rudia chorus:
BRIDGE:
Sitaki leo kuwa historia
Labda kesho iwe historia
Nataka niache historia
Itakapofika kuwa historia
(Visited 2 time, 1 visit today)
Previous Post Next Post