Mama yake Young Killer adai alimpiga sana mwanae alipoanza kurap akiwa darasa la tatu, "mwisho wa siku alituzidi ujanja"

Rapper toka Mwanza, Young Killer Msodoki alijikuta katika wakati mgumu kutokana na kuanza kuonesha makali ya kipaji chake mapema akiwa shule ya msingi tena darasa la tatu.

Mama mzazi wa rapper huyo, aliiambia Bongo Dot Home ya 100.5 Times Fm kuwa hakupenda kabisa kumuona mwanae anaanza kujiingiza katika masuala ya kisanii hivyo alishirikiana na kaka zake kuhaikisha wanaikomesha tabia hiyo.




“Yaani sikuwahi kumsapoti hata siku moja, yaani nilimpiga sana kuhusiana na hilo suala la kuwa msanii.”Alisema mama Msodoki. “Sikutaka kwamba asiwe msanii, nilipenda lakini sasa nilitaka asome amalize shule then angeendelea na masuala yake.”

“Alianza hayo masuala akiwa bado darasa la tatu au la nne kama sikosei. Alianza siku nyingi sana. Tumempiga sana hata kaka zake walimpiga sana lakini mwisho wa siku alituzidi ujanja.” Aliongeza mama Msodoki.

Hata hivyo, alisema baada ya kugundua kuwa ni kipaji chake, sasa hivi anampa sapoti na anamuombea kwa Mungu amsaidie aendelee vizuri katika muziki wake na ampe afya nzuri.

Alieleza kuwa hivi sasa anaona faida kubwa kwa mwanae ambaye anasaidia sana familia na kwamba hadi sasa kuna nyumba anayoendelea kuijenga.

Mama aliwafurahisha wengi pale alipoulizwa na One B aka Moko Biashara kuimba mistari ya Young Killer anayoifahamu na ndipo mama Msodoki akatupia mistari miwili mitatu ya ‘Dear Gambe’ ya Young Killer.

Previous Post Next Post