RAIS KIKWETE KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 25 YA HOSPITALI YA KAIRUKI, DAR ES SALAAM, LEO

hk1Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt Salim Ahmed Salim wakiangalia watoto wachanga waliotunzwa katika chumba maalum muda mfupi baada ya kuzaliwa wakati Rais Kikwete alipotembelea sehemu mbalimbali za hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki akiwa mgeni rasmi katika sherehe za miaka 25 ya kuanzishwa kwake leo Machi 16, 2013.

 hk10
Baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria  sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013   hk12

Rais  Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi tuzo kwa kutambua mchango wake mkubwa katika sekta ya afya nchini wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali hiyo leo Machi 16, 2013   hk15
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013

hk17Seehemu ya wageni waalikwa na wanafunzi na wafanyakazi wa hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013 hk18Msanii Mrisho Mpoto akiburudisha wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013 hk19
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wakikata utepe kuzindua rasmi hosteli ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki  wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013 PICHA NA IKULU
………………………………………………………………………….
RAIS Jakaya Kikwete amewataka Watanzania kuiunga mkono serikali katika jitihada zake za kuwasogezea karibu huduma za afya wananchi popote walipo nchini.

Kauli hiyo aliitoa jijini Dar es Salaam jana, wakati wa maadhimisho ya miaka 25 ya utoaji huduma za afya, katika hospitali ya Hubert Kairuki.

Alisema serikali imejipanga vizuri katika kuzijengea uwezo hospitali kwa kuongeza madaktari, ili kuondokana na changamoto zinazowakabili kwa kuwahudumia  wagonjwa wengi kwa wakati mmoja.
Kikwete alisema mipango wa ujenzi wa Chuo cha Mlogazila imekamilika, ambacho kinatarajiwa kuzalisha wataalamu 12,000 kwa mwaka kitakapoanza.

“Kuna watu kazi yao ni kukebehi kila kinachofanywa wakidhani kuwa  kama wangekuwa wao wangeweza kufanya kirahisi, bila kujua kila kinachofanyika kina mchakato wake hata hivyo, sisi tutafanya”alisema Kikwete.

Kikwete alisema hivi sasa serikali inakusudia kuziimarisha hospitali zote hapa nchini ili kuondokana na tabia ya kuwasafirisha wagonjwa kwenda nje kwa ajili ya baadhi ya matibabu.

Aidha, aliupongeza uongozi wa Hospitali hiyo kutokana na juhudi zake za kutoa huduma hiyo ya miaka 25 bila kutetereka ambapo pia imeanzisha kituo cha kupambana na kuzuia vifo vya watoto pamoja na akina mama wajawazito.

Vilevile alizitaka hospitali hizo za binafsi kujitahidi kuboresha huduma zake hadi zilingane na huduma zinazotolewa katika nchi za nje kama vile India.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Asser Mchomvu alisema tangu kuanzishwa kwake iliweza kuhudumia wagonjwa milioni tatu.

Alisema mafanikio hayo yalitokana na ushirikiano uliyojengeka kati ya wafanyakazi wa hospitali hiyo, kuanzia ngazi ya chini hadi juu.
Previous Post Next Post