Jaji Warioba awasilisha rasimu ya katiba, adai muundo wa serikali mbili hauwezi kubaki

Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba amewasilisha rasimu ya katiba katika bunge maalum la katiba.



Jaji Warioba amewasilisha rasimu hiyo leo bungeni mjini Dodoma kushindwa kufanya hivyo jana kutokana na baadhi ya wajumbe wa bunge hilo kupinga uvunjaji wa kanuni wakitaka Rais Jakaya Kikwete azindue bunge hilo na kisha rasimu kuwasilishwa.

Akizungumzia suala la muungano katika hotuba yake, Jaji Warioba ameeleza kuwa muundo wa serikali mbili tulionao sasa hivi hauwezi kubaki kwa kuwa muungano waliouacha waasisi sio muungano tulionao hivi sasa.

amesema kuwa wakati wa kukusanya maoni, asilimia 61 ya wananchi wa Tanzania Bara waliopata nafasi ya kutoa mapendekezo walitaka kuwepo muundo wa serikali tatu, huku asilimia 60 ya waliotoa mapendekezo Zanzibar walitaka muungano wa mkataba.
Previous Post Next Post