COMMEY NA MOHHAMED WATAMBIANA


2 1faf3
International BoxingFederation Africa
IBF/AFRICA
FOR IMMEDIATE RELEASE – Friday, March 1st, 2013 -Dar-Es-Salaam, TANZANIA- Mabondia wawili wanaotarajia kupigana kesho Ijumaa ratehe 8 Machi kugombea ubingwa wa Afrika katika uzito wa Lightweight, Richard Commey na Bilal Muhammed  wamekutana leo katika zoezi la kupima uzito na nusura wazipige kavukavu kama wasingeachanishwa na wasimamiszi wa mpambano huo.
Richad ndiye aliyekuwa wa kwanza kuwasili katika eneo la kupima uzito ambalo ni hoteli maarufu ya Coco Grove Regency iliyoko karibu na uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kutoka jijini Accra. Alifuatana na meneja/promota wake Michael Amoo- Bediako na kocha wake Carl Lokko.

Bilal naye aliingia muda mfupi baadaye akifuatana na meneja pamoja na kocha wake Yebohey na kundi kubwa la mashabiki wa kambi yake kutoka Bukom, Jamestown.
Mabondia wote Richard na Bilal walifikia uzito wa kilo 59.9 na kutangazwa kufikia uzito unaokubaliwa na IBF katika uzito wa mwepesi. Zoezi hili lilisimamiwa na Mtanzania Onesmo Ngowi ambaye ndiye Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati akisaidiwa na referii Rodger Barnor wa Ghana.
Mpambano huu utafanyika kesho tarehe 8 Machi katika ukumbi wa Will Power Gym – City Engineers, Jamestown jijini Accra ambapo Mfalme wa uzito mwepesi katika bara la Afrika atajulikana rasmi.
ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA
Previous Post Next Post

Popular Items

Kenya katika hatari ya kupata Ebola

Picha: Soggy Doggy Aongeza Familia