Audio: Mama yake Roma anapenda nyimbo za Linex kuliko za Roma ila uvaaji wake wa suruali 'mlegezo' unamsononesha

Ingawa Roma Mkatoliki anaishika Tanzania kwa nyimbo zake na kueleweka sana kwenye masikio ya watu wengi hasa vijana, mama yake mzazi sio shabiki wake mkubwa na anawakubali waimbaji wengine zaidi yake.

Rapper huyo toka Tanga ameeleza kupitia kipindi cha Bongo Dot Home cha 100.5 Times Fm wakati anapiga story na Jabir Saleh, Moko Biashara na Godzilla.




Roma amemtaja Linex kuwa kati ya wasanii watatu ambao mama yake mzazi anawapenda zaidi lakini siku zote analalamikia uvaaji wake wa suruali.

“Bibi Mkubwa kwanza mimi anawasanii watatu ambao anawakubali sana. Anapempenda Sunday Linex, anampenda Barnaba…huwa anasema ‘yaani Linex mimi na mpenda sana sema mlegezo tu, hapo ndo ananivuruga hapo anashindwaje kupandisha.” Ameeleza Roma Mkatoliki. “Nakwambia Linex akiperform anatamani akimbie akabebe suruali aipandishe.” Aliongeza kwa utani.

Mkali huyo wa ‘KKK’ amewataja wasanii ambao wanapendwa zaidi na mama yake ukiacha Linex ambaye ndiye ‘favorite artist’ wake kuwa ni Barnaba, Bushoke na Ben Pol.

Lakini inapokuja kwenye suala la kusikiliza rap za Rhymes Of Magic and Attraction (R.O.MA), bado mama hajazielewa.

“Mimi mother naona hanielewagi, naonaga hanielewagi. Labda nilete mpunga ndo kidogo anacheka kwamba mwanangu unaimba vizuri lakini naonaga kama sio big fan wangu. Kwa sababu mimi naweza kukaa home nasikiliza mangoma, labda namsikiliza mwanangu Ben Pol anavyorindima unaoma kabisa mama anafeel kabisa eeeh, lakini labda Mr. President ikaanza pale ‘Ikulu’ unasikia eeeh hebu punguzeni sauti, nyimbo nyingine zina kelele, unaona hapa kama mama kakaza daah.”

Msikilize hapa:







Previous Post Next Post