Mustapha aomba radhi baada ya Nyota Ndogo kuongoza maandamano kupinga tabia zake kuwa zinadhalilisha wanawake

Suala la msanii wa Kenya, Colonel Mustapha kupost picha akiwa na Huddah Monroe zilizoweka alama nyingi za kuuliza kwa wana maadili limeendelea kuwa mwimba kwake.



Siku kadhaa baada ya Huddah kudai kuwa hawana uhusiano wowote na Mutapha zaidi ya kupiga picha ili kumpa kick msanii huyo, wanawake wa Pwani wakiongozwa na mwimbaji wa kike wa Kenya Nyota Ndogo waliandamana wakilaani vitendo vya Colonel kwa madai kuwa amewadhalilisha wanawake.



Wanawake hao walikuwa na mabango yaliyoondikwa “Colonel Mustapha heshimu wanawake, Mustapha Komesha dhuluma kupitia mtandao heshimu muziki, Wanawake ni dada zako na mama zako,” na mengine.

Mustapha ameguswa na maandamano hayo na ameomba msamaha wakati anaongea na mtangazaji maarufu Mzazi Willy M. Tuva.

“Ninawaomba msamaha kwa sababu ni lazima tu-respect wamama.”
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA