Balozi Fulgence Kazura Afariki Dunia

Aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Balozi Fulgence Kazaura enzi za uhai wake akimtunuku PhD Waziri wa ujenzi Dk. John Magufuli.

Sima Kazaura anasikitika kutangaza kifo cha baba yake mzazi Balozi Fulgence Kazaura aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam (UDSM) kilichotokea leo nchini India. Kama ilivyo ada kupeana mkono wa pole na kufarijiana ndio ustaarabu wetu wakatio wa msiba hapa DMV.

Msiba upo 21, Featherwood Court Apt. 14
Silver Spring MD 20904
Tutazidi kuwajuza mambo yanavyoendelea katika msiba huu hapa DMV na nyumbani Tanzania. Chini hapo ni namba ya mfiwa.

Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu.
Sima Kazaura 202 413 9184

Bwana ametoa, Bwana ametwaa na jina lake na lihimidiwe.
Amina


Source:GlobalPublishers
Previous Post Next Post