Malori mawili yamegongana kwenye mlima uliopo eneo la kijiji cha Fulwe, kata ya Mikese, mkoani Morogoro na kulipuka moto.
Ajali hiyo, imehusisha malori mawili moja likitokea upande wa Dar likiwa na shehena ya mafuta na lingine semitrela lililokuwa likitokea upande wa Morogoro.
Dereva wa lori la mafuta ameteketea kwa moto wakati wa semitrela na tingo wake wakinusurika na kukimbizwa hospitali.
Tazama picha hapa chini za ajali hiyo....
Baadhi ya watu waliokwama kijiji cha Fulwe kata ya Mikese mkoani Morogoro wakiangalia mwili wa dereva wa lori lililobeba shehena ya mafuta lililokuwa likitoka Dar kueleka upande wa Morogoro, ukiwa umeteketea vibaya kwa moto baada ya ajali.
Mwili wa dereva wa lori la mafuta ukiwa umeteketea kwa moto.
Wananchi wakibeba mwili wa dereva wa lori ulioteketea kwenye moto.
Source: GPL, MOROGORO