Prezzo na Cannibal wakanusha kuzinguana

Kumekuwepo na tetesi kwa miezi ya hivi karibuni kuwa wasanii wa label ya Makini Music Group, Prezzo na Cannibal wamevunja uhusiano wao. Hata hivyo wakiongea na mtandao wa Nairobi News, wote Prezzo na Cannibal wameweka wazi kuwa bado wanafanya kazi pamoja.



Cannibal, alijiunga na MMG miaka mitatu iliyopita na kuhamia Nairobi kutoka Mombasa na alikuwa msanii wa kwanza mkubwa kusainishwa Prezzo baada ya kuivunja Cash Money Brothers. Baada ya hapo waliachia single yao My City My Town, wimbo uliokuwa ukisifia miji ya Nairobi na Mombasa.

“Bado nafanya kazi na Prezzo na hakuna ugomvi kati yetu. Tuna projects zaidi zinakuja,” alisema Cannibal. Hata hivyo wasanii wengi waliojiunga na MMG, wanadaiwa kujiondoa.
Source: Nairobi News

Previous Post Next Post