Picha: Birdman Jr. Jr. Tyga anunua gari lenye thamani ya shilingi bilioni 3.5, awa sawa na jay z pamoja na Berdmen

Rapper wa YMCMB, Tyga amenunua gari la kifahari lenye thamani ya dola milioni 2.2 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 3.5 na kwa sasa fans wake wanamuita Birdman Jr. Jr.

 Vyanzo vilivyo karibu na Tyga vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa Tyga amenunua gari hilo aina ya ’2014 convertible Maybach 62 S Landaulet’ lenye thamani ya $1.3 mil. Hata hivyo, Tyga ametumia karibu dola milioni 1 kulipamba.


 Kampuni maarufu ya West Coast Customs imeipimp gari hiyo kwa kuongeza vitu mbalimbali ikiwemo TV yenye inch 40.
Tyga anaungana na Jay Z na Bird Man wanaomiliki gari aina hiyo. Inasemekana kuwa Tyga amepanga kuionesha gari hiyo kwenye video yake ya “Wake Up In It.”




Previous Post Next Post