Young Jeezy akamatwa kwa kumpiga mwanae

Young Jeezy anaunza mwaka mpya vibaya. Rapper huyo amekamatwa huko Atlanta, Marekani kwa makosa ya kutumia nguvu (battery), kumshikilia mtu ndani bila ridhaa yake (false imprisonment) na kutoa vitisho vya kigaidi dhidi ya mwanae wa kiume.


Kwa mujibu wa TMZ, Rapper huyo mwenye miaka 36 aliyezaliwa kwa jina la Jay Jenkins, aliingia kwenye ugomvi na mwanae bafuni September 2012. Katika ugomvi huo, anadaiwa kumtupa mwanae kwenye mlango wa vioo wa bafuni, kumpiga ngumi usoni, kumburuza hadi chumbani na kuanza kumpiga.

Kwa mujibu wa nyaraka za polisi, Jeezy alikuwa akisikika akiamwambia mwanae: I will kill you.” I will put a bullet in your head right now. If I could get away with it, I would kill you.” Jeezy alijisalimisha mwenye kwa mamlaka husika Ijumaa iliyopita na alitolewa kwa dhamana ya $45,000.

Hata hivyo kwa mujibu wa TMZ, Young Jeezy anasema hakumpiga mwanae wala kutoa vitisho hivyo na kwamba mambo yote hayo yamepangwa na mama wa mtoto wake, Tenesha Dykes, ambaye anamuita ni mtu mwenye tamaa na mpenda fedha.
Vyanzo vilivyopo karibu na rapper huyo vimeuambia mtandao huo kuwa Jeezy na mwanae huyo mwenye miaka 17 aitwaye Jadarius kuwa kweli waliingia kwenye mabishano makali Sept., 2012, lakini hayakuwa makubwa kiasi cha wawili hao kutwangana kama ilivyoripotiwa.

Inasemekana kuwa yote hayo yalianza baada ya Jeezy kumwambia mwanae amekuwa na tabia mbaya na kwamba hakutaka aishi kwenye nyumba yake.


Previous Post Next Post