Picha: Uzinduzi wa kitabu cha Faraja Nyalandu 'Unaweza'

Aliyekuwa miss Tanzania 2004 ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa taasisi ya Shule Direct, Faraja Nyalandu Kotta Jumatano hii amezindua kitabu chake kipya ‘Unaweza’ kwaajili ya wanafunzi wa shule ya msingi.



Faraja akimwonesha mwanafunzi sehemu ya kusoma

Katika uzinduzi huo uliofanyika katika Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es salaam ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu, pamoja na rafiki zake Miss Tanzania wa mwaka 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe aka ‘K-Lynn, na Nancy Sumari, Miss Tanzania 2005.

Akizungumza na katika uzinduzi huo Faraja Kotta amesema kitabu hicho kinalenga kusaidia wanafunzi kujenga uwezo na maarifa ili kumudu masomo yao.

“Kitabu cha ‘Unaweza’ Mbinu kumi za kumudu masomo yako, kilizaliwa kwasababu nimeona kuna haja ya wanafunzi kuhimili changamoto za uanafunzi na kufanikisha vyema azma ya kwenda shule. Tunajifunza kila siku,kuna wakati tunajua kwamba hapa sasa tunajifunza na kuna wakati hatujui kwamba tunajifunza.Ni muhimu kujenga misingi hii ya kujifunza mapema,” alisema Faraja.

Pia Faraja amewapongeza wanafunzi wote wanaotambua umuhimu wa kutumia maktaba,akisema ni mfano wa kuigwa.

Aidha Faraja ametoa wito kwa watu mbalimbali wenye mapenzi mema na elimu kuhifadhi upatikanaji wa kitabu cha ‘Unaweza’ kwenye maktaba nyingine za mikoa na wilaya.Huku akisema asilimia 50 ya mauzo ya kitabu cha ‘Unaweza’ yataenda Chuo cha Ualimu cha Korogwe,hususan chumba cha Teknohama kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa elimu wa teknolojia.


Baadhi ya picha kaika uzinduzi wa kibau cha Unaweza.




Faraja akizungumza

Faraja Kotta akiwa na Jacqueline Ntuyabaliwe

Faraja Kotta akimwambia kitu Nancy Sumari

Faraja na Lusajo

Faraja na Nancy


Jacqueline Ntuyabaliwe

Nancy Sumari


Faraja Kotta akiwa na Mkutubi wa jiji Misekelo Mwalugelo

Wadau walioudhuria uzinduzi huo

Wadau walioudhuria uzinduzi huo



Previous Post Next Post