Unataka kuijua siri moja wapo ya mafanikio ya msanii Diamond Platnumz na watu wengine maarufu waliofanikiwa, ni kutafuta njia ya kurudisha katika jamii sehemu ya kile wanachokipata kupitia kazi zao.
Mwaka jana mwishoni Abdul Naseeb a.k.a Diamond aliweka ahadi ya kuwasomesha watoto walioshiriki na kushinda shindano la kucheza Ngololo, katika show ya watoto iliyofanyika Leaders club siku ya Christmas.
Jana (January 21) hit maker huyo wa ‘Number One’ amepost picha akiwa East Africa International School iliyoko Mikocheni, Dar es salaam ambapo ndipo watoto hao walioshinda watasoma kwa kulipiwa ada na Diamond.
“siku niliyopanga kutimiza ahadi yangu ya Kuwapeleka shule watoto walioshinda shindano la kucheza ngololo..na kwa vile nilitaka wapate elimu iliyo bora zaidi, nilikaa na management yangu..na kutafiti ni shule ipi itakayokidhi mahitaji ya watoto wale,shule yenye mazingira mazuri ya kusomea na yenye standard nzuri. sote tulikubaliana kuwapeleka shule ya EAST AFRICA INTERNATION SCHOOL,iliyopo Mikocheni. napenda kumshukuru mkuu wa shule hii,Bi Mercy Githirua kwa kutupokea vizuri mimi na watoto wale..lakini pia kuwashukuru wanafunzi wote kwa kutupokea vizuri”, aliandika Platnumz kupitia website yake.
Akiwa katika ofisi ya mwalimu mkuu wakati wa kuwaandikisha watoto hao
Watoto waliopata bahati ya kusomeshwa na Diamond
Picha: This Is Diamond