PICHA: MAYWEATHER 'ALIVYOWATANDIKA' PACQUIAO, AMIR KHAN NA MAIADANA

Bondia Floyd Mayweather amefufua vita ya maneno na mpinzani wake, Manny Pacquiao pamoja na kuwakandia pia Amir Khan na Marcos Maidana kwa staili ile ile. Pamoja na kumuita Pacquiao majeruhi wa Juan (Manuel) Marquez akikumbushia kipigo cha Mfilipino huyo mwishoni mwa mwaka 2012 kwa Knockout (KO) kutoka kwa Mmexico huyo, Mayweather ameweka picha ya 'kubumba' akiwa amemsukumia konde zito usoni. "Sasa unaniambia nakwenda kula makombo ya Juan Marquez? Acha nizungumze na IRS juu ya hili," alitweet mbabe huyo.


 Floyd Mayweather (kushoto) akimsukumia konde Manny Pacquiao, kuashiria pambano baina yao linaweza kuokea Awali iliripotiwa, Khan anajiandaa kuwa mpinzani ajaye wa Mayweather mwezi Mei, lakini Mmarekani huyo ameendelea kuwaambia mashabiki wake kwamba ataendeleza ubabe wake.Kama ambayo wengi wanchukulia Khan atakuwa mpinzani dhaifu kwa Mayweather, bondia huyo naye amembeza akimuita 'Con Artist' katika picha ambayo amebandika ya kubumba akimchapa konde hadi kuelekea sakafuni. Amesema: "Hebu fikiria, nini Amir "Con Artist" atapata kama atachaguliwa kuingia anga za Mayweather,". Mtu mwingine anayechukuliwa kama mpinzani wa baadaye wa bondia huyo bingwa wa madaraja matano ya uzito duniani ambaye hajawahi kupigwa ni Muargentina, Maidana, kufuatia ushindi wake wa kushitua dhidi ya mbabe aliyepewa jina 'New Mayweather', Adrien Broner. >Akiwa amebandika picha kama hizo,akimtandika ngumi ya mkono wa kulia, Mayweather pia ametweet kuhusu bondia huyo: "Naweza kuagiza kipande kimoja na biskuti tafadhali? Hakuna sehemu."
Sakafuni: Floyd Mayweather ameweka picha akimuadhibu Muingereza Amir Khan, pambano lao linatarajiwa kufanyika Mei
Konde la nguvu: Lakini Floyd Mayweather anajiamini pia atampiga Marcos Maidana (kushoto)
Mfalme wa masumbwi: Floyd Mayweather amekuwa akipewa heshima ya bondia bora kwa muda mrefu
Previous Post Next Post

Popular Items