Masogange Kuwa Video Queen wa video ya ‘Msambinungwa’ Ambayo Itafanyika Kenya

Video Queen wa Bongo, Agness Gerald aka Masogange’ Pamoja na Tunda Man ,Ali Kiba wanatarajia kwenda nchini Kenya kushoot video ya wimbo mpya ya Tunda Man ‘Msambinungwa’.
 



Tunda amesema ameamua kwenda kuandaa video yake nchini Kenya kutokana na kampuni hiyo ya video kusambaza video zao wenyewe katika TV kubwa zote Afrika.

“!Nimeamua kufanya kazi na Pink Lab ili kufanya kitu tofauti na production za Bongo, kwasababu ukifanya video na hao jamaa suala la usambazaji ni juu yao,kwahiyo safari hii tunaweza tukaonekana Channel O na TV zote kubwa za Afrika,” alisema Tunda.

Tunda amesema ingawa ni gharama kubwa sana kutengeneza video na kampuni ya Pink Lab, imembidi afanye hivyo ili apate kile ambacho kitakuwa kizuri zaidi. “Siwezi sema video itagharimu kiasi gani kwa wakati huu,kwahiyo nasubiria mpaka mambo yakishamalizika ndipo naweza nikasema kiasi gani nimetumia, ila ni pesa nyingi.”

Previous Post Next Post