Beyonce Atoa Album yake ya 5 Kupitia iTunes Pekee

Mama wa Bule Ivvy Beyonce amewashtukiza mashabiki wake kwa kuachia album mpya kwenye mtandao wa iTunes bila kutangaza. Album hiyo ya 5 imepewa jina lake mwenyewe, ‘Beyonce’ na inafahamika kama “Visual Album” kwakuwa kila wimbo una video yake.


MTV walitweet: It’s official, Beyonce just won the internet.”

Record label yake, Columbia records, ilitweet leo, “#Beyonce The Visual Album. 14 songs 17 videos available now on iTunesMusic.”

Kwenye album hiyo, Beyonce ameishirikisha pia familia yake, yaani mumewe Jay Z na mwanae Blue Ivy. Wengine walioshirikishwa kwenye album hiyo ni pamoja Drake na Frank Ocean.

Beyonce bado hajatweet chochote kuhusiana na album yake lakini mdogo wake Solange ametweet: “So my sister is a f—ing G. Beyonce, the visual album out now.”
Previous Post Next Post

Popular Items