Muigizaji wa BongoMovies, Irene Uwoya amesema kupitia kipindi chake cha Paradise ambacho husaidia kuzifanyia ukarabati nyumba za Watanzania zilizo na hali duni, amesema kipindi hicho kimemfanya aione picha halisi ya jinsi Watanzania wengi wanavyoishi katika umaskini mkubwa.
Irene amesema ni ngumu kuyajua maisha ya mtu umwonapo barabarani lakini ukienda anakoishi ndiko utakapoujua ukweli.
“Nimegundua kwamba asilimia kubwa ya Watanzania wanaishi katika mazingira magumu, mabaya sana kuliko unavyotegemea,”amesema Irene. “Unaweza ukakaa na mtu unapiga naye story, kumbe kwake anakoishi ana maisha magumu kwelikweli,”ameongeza.
“Kwahiyo mimi navyotembea hivi nakutana na vitu vingi na nimejifunza mengi. Mimi nikikaa kwangu naona niko sawa, wengine wanakuwa hawana hata sehemu ya kwenda choo, mtu akitaka kwenda chooni anachimba shimo kwa jembe. Nimejifunza vitu vingi ambavyo nilikuwa sivijui vinaendelea katika hii nchi.
Akiongelea changamoto za kipindi hicho, Irene amesema wapo watu wamekuwa wakimpigia simu na kumponda kuwa ameacha kujenga kwao na ameamua kusaidia watu wasio ndugu zake. Changamoto nyingine ni kukutana na watu wanaojifanya wanashida kumbe ni wasanii tu.
“Kuna nyumba moja tulienda yule mama akaelezea mpaka akalia lakini kumbe sinema tu, hana matatizo wala nini,” amesema Irene.
Ameeleza kuwa wakati mwingine hukutana na watu wenye matatizo makubwa ambayo wakimuelezea hujikuta yakimgusa kiasi cha kumliza na kushindwa kurekodi kipindi.
“Mara nyingi kila nikienda sehemu unakuta mtu ananihadithia mpaka nashindwa kushoot machozi yananitoka, yaani kiukweli nakuwa naumia. Karibia scenes kibao nashindwa kushoot sababu ya hiyo.”