PICHA: MEYA JERRY SILAA ATINGA KWA WACHORAJI WANAOMUUNGA MKONO KATIKA ZOEZI NA KAMPENI YA "DAWATI NI ELIMU"

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaa, Jerry Slaa amewatembelea wachoraji wa picha ambao picha zao zitauzwa kwenye mnada maalum wa kuchangisha fedha za kununulia madawati yatakayotumika kwenye shule za manispaa hiyo. Mpango huo ni sehemu ya kampeni yake ya ‘Dawati ni Elimu’


Meya Jerry Slaa akiangalia moja ya picha zilizokamilika na zilizochorwa na mchoraji wa Tanzania

Kampeni hiyo imepanga kukusanya shilingi bilioni 4.98 zitakazotumika kununulia madawati kwenye shule za msingi na sekondari 30,487 katika manispaa ya Ilala kwa mwaka wa fedha 2013/14.


Mchoraji akilichora soko la Kariako, wanaotazama ni Meya Slaa na Mkurugenzi Mtendaji wa 361 Mustafa Hassanali

Picha hizo zitauzwa kwenye mnada wa hisani utakaofanyika Hyatt Regency Kilimanjaro Hotel Jumamosi hii ya November 16.

                                
                                                 Mchoraji Haji Chilonga akiwa kazini

Jumla ya wachoraji 10 wameshiriki kuchora picha mbalimbali.


                        Meya Slaa akiongeza kitu kwenye picha iliyochorwa na Poni Yengi


                            Meya Jerry Slaa akimtazama mmoja wa wachoraji 10 wanaoshiriki

Wachoraji wanaoshiriki ni:

– ROBINO NTILA
– AGGREY MWASHA
– SALUM KAMBI
– CUTHBERT SEMGOJA
– JAMES HAULE
– HAJI CHILONGA
– THOBIAS MINZI
– MOSES LUHANGA
– PONI YENGI MISS
– VITA MALULU
Previous Post Next Post

Popular Items