PICHA: BILIONEA KUTOKA UK , RICHARD BRANSON AZINDUA KIOTA CHAKE CHA KIFAHARI NA GARAMA "MAHALI MZURI" MASSAI MARO

Bilionea wa nchini Uingereza, Sir Richard Branson hivi karibuni alikuwa mwenyeji wa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwenye kiota chake kilichopo ndani ya mbuga ya Maasai Mara.

Kiota hicho kiitwacho ‘Mahari Mzuri Safari Camp’ kilifunguliwa rasmi weekend iliyopita na kupewa baraka na wazee wa kabila la Wamasai.
Mahali Mzuri inajumuisha mahema 12 ya kulala yaliyopewa jina la makundi 12 ya kabila Maasai kwenye eneo hilo.
Ingawa hoteli hiyo ilikuwa imeanza kazi tangu mwaka 2003, Branson aliizindua rasmi kwa kuwaalika wazee wa kabila hilo kubariki huku tayari Branson akiwa anatumbulika kama mzee wa kabila hilo tangu miaka minane iliyopita.



Gharama za kulala kwa usiku mmoja zinaanzia $590 kwa mtu mmoja
Previous Post Next Post

Popular Items