IRENE PAUL WA BONGO MOVIE AFUNGUKA JINSI ANAVYOFANANISHWA NA ANGELINA JOLIE

Huwaga Wanasema duniani kuna watu kama sita hivi wenye sura kama yako na pia waswahili wanasema duniani wawili wawili. Na ndio maana usishangae kukutana na muigizaji mrembo wa Tanzania, Irene Paul na ukagundua kuwa kuna kitu anachofanana na muigizaji maarufu wa Marekani, Angelina Jolie.

Watu wengi wananiambia hivyo kwamba nimefanana naye, hata mimi mwenyewe some features. It’s true, she is my role model lakini kuna some features ambazo nimefanana naye na nilishafanyiwa interview nikajikuta kwamba ni kweli ninafanana naye. Nimefafana naye midomo, taya (jaws), macho, vitu kama hivyo,




Irene amesema ana ndoto pia za kuja kuwa muigizaji wa filamu za action kama anazofanya Angelina Jolie zikiwemo Wanted, Salt, Mr & Mrs Smith, Lara Croft: Tomb Rider na zingine.

“Natamani kubadilisha tasnia ya Tanzania sana sana kwa sisi wasichana kwasababu sijaona mtu anayefanya kitu kama hicho, siku moja naamini ntaweza,” alisema Irene na kuongeza kuwa filamu nyingi za Tanzania ni za mapenzi.






News Via: Bongo5 
Previous Post Next Post

Popular Items