Muziki wa Bongo Unalipa: Wampatia Rich Mavoko Gari na Nyumba

Hit maker wa Roho yangu, Rich Mavoko amesema ameanza kupata mafanikio makubwa katika muziki wake baada ya kununua gari aina ya Nissan pamoja nyumba ambayo bado anaendelea kuijenga mkoani Morogoro.




                               Hii ndio Nyumba ya Rich Mavoko ambayo ipo Morogoro

“Sina cha kusema muziki unalipa, nyumba yangu ni kubwa sana na pia nimejaribu kuonyesha ni mafanikio gani ambayo nimeyapata mpaka sasa. Kwahiyo namshukuru Mungu na mashabiki ambao wananiwezesha,” amesema Mavoko.

                                           Na Hii ndiyo Gari ya Rich Mavoko.

“Wapo ambao walipata bahati kama yangu wakashindwa kuitumia, kwa mimi nimetumia nafasi niliyoipata, ndio maana nafanya mambo makubwa kama ninavyoingia gharama ya laki 8 kwajili ya mavazi kwenye shoo zangu kubwa. Kila show kubwa natoa laki 8 kwa mbunifu wangu.”

Aliongeza kuwa muziki hauna bahati bali ni kujituma.
Previous Post Next Post