Picha: Makamu wa Rais aongoza shughuli za Kumuaga Marehemu Julius Nyaisangah Leo Leaders

Makamu wa Rais Dr. Mohamed Gharib Bilal leo amewaongoza wakazi wa Dar es Salaam, kuuaga mwili wa aliyewahi kuwa mtangazaji wa Radio Tanzania, Radio One na kuwa Meneja wa Abood Media, Julius Nyaisangah aliyefariki dunia juzi mkoani Morogoro.

Makamu wa Rais Dokta Gharib Bilal

Wengine waliokuwepo kuuaga mwili wa marehemu Nyaisangah ni pamoja na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Freeman Mbowe, Mkuu wa wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa na mumewe Boniface Mkwasa.

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi akiuaga mwili wa marehemu Nyaisangah

Aliyewahi kuwa mtangazaji wa Radio One ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa akiwa na mume wake Boniface Mkwasa

                              Betty Mkwasa akiuaga mwili wa marehemu Julius Nyaisangah

                                           Familia ya marehemu Nyaisangah


                                   Godwin Gongwe na Ruge Mutahaba waliokaa katikati

                           Mengi akiuaga mwili wa marehemu Nyaisangah

                 Reginald Mengi, Makamu wa Rais Dr. Bilal, Betty Mkwasa na Freeman Mbowe

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi akisalimiana na Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal






Marehemu Nyaisangah atazikwa wilayani Tarime, Mara.

Image Credit: Dewjiblog 

Previous Post Next Post

Popular Items