Kampuni Kubwa Duniani ya Sony Music Afrika itamsaini msanii wa pili wa Tanzania atakayeungana na Rose Muhando mwishoni mwa mwaka huu.Mkurugenzi na Mkuu wa Vipaji na Biashara Mpya Afrika wa Rockstar 4000 / Sony Music Africa, Seven Mosha ameiambia Bongo5 kuwa msanii huyo atatangazwa baada ya nyimbo za Rose Muhando aliyesainishwa February mwaka jana zitakapoanza kutoka.
Seven Mosha (Kulia) akiwa na Vanessa Mdee
Akielezea vigezo wanavyotumia kuwasainisha wasanii kwenye label hiyo, Seven amesema mara nyingi hawachukui wasanii wasiojulikana kabisa na hutumia zaidi mtandao kujua msanii anayefaa.
“Kila Jumatano huwa tuna meeting inayoitwa A&R ambayo wanaangaliwa wasanii wote waliopo online,” amesema Seven. “Kitu cha kwanza ambacho huwa tunaangalia ni online. Ntachukulia mfano Xtatic. Ilikuwa ni kazi aliyoitoa as underground akaweka video yake online and the alikuwa hajulikani, hana deal yoyote lakini kukawa kuna watu wameupenda wimbo wake, wameappreciate talent yake.”
Xtatic – rapper wa Kenya
“Basi tukiona hivyo na tukiangalia overall vitu vingine vinakaa sawa, unakuta labda Xtatic ni mtu ambaye ana muonekano mzuri, anaandika nyimbo zake mwenyewe, anaweza kuimba lugha tofauti, labda anaweza kuplay instruments vilevile. Kwahiyo inakuwa ni mtu ambaye ni rahisi sana kumwekea investment, ni rahisi sana kumuuza. Lakini unakuta kuna wengine ambao wameshaanza kibiashara kwa lengo fulani , ndio watu kama D’Banj, kama Rose Muhando, unaona kwamba hiki ni kipaji kitakakaa kwa muda fulani, kwahiyo sisi tukiongeza ujuzi wetu tutaenda mbali pamoja naye.”
Seven amesisitiza umuhimu wa wasanii kupatikana mtandaoni kwakuwa ni kigezo kikubwa zaidi.
“Muda mwingi sana tunautumia online, different websites, different Youtube links. Saa zingine kwenye Twitter unakuta mtu amemrecommend sana mtu huyu, tunasikiliza nyimbo. Kama tunakupenda tukupigia simu, first meeting inafanyika, tunaangalia kama una malengo kama yetu, basi unasainishwa. Digital platform ni kitu kikubwa sana kwetu. Ndio tunaangalia sana vitu vingi huko.”

Tags:
Entertainment