DAR BURUDANI ZA KUFA MTU "NOV 9 FIESTA NOMA SANA ..JUKWAANI UTAWAKUTA WAKALI HAWA "MAHOMBI, IYANYA,ALAINE,DAVIDO,MI CASA" NA NOV 23 NI P-SQUARE..GET READY TO PARTY

October na November ni miezi ambayo kwa Dar es Salaam, Chrismas na mwaka mpya zitakuja mapema.






Itaanza Serengeti Fiesta Dar es Salaam, ambapo Naija Music itashutdown mitaa ya Dar es Salaam pale ambapo wasanii wa Nigeria, Davido, Iyanya na J-Martins watashare stage moja la Fiesta.


Davido


Iyanya

Ngoma zao, Demiduro, Kukere, Touching Body zitatumbuizwa live.

Hiyo itakuwa ni nusu tu ya burudani ya Fiesta, sababu mrembo kutoka Jamaica, Alaine na msanii wa Sweden, Mohombi wataungana na Wanaijeria hao kuzikata kiu za wapenzi wa burudani wa Dar es Salaam.

Alaine




Mohombi

Hits kama Sacrifice na Without you za Alaine na Bumpy Ride na Coconut Tree zitapigwa live.

Baada ya shangwe za Fiesta, joto la burudani litarejea tena November 9 ambapo Dr. Duda, J-Something na Mo-T wa bendi ya muziki wa house ya Afrika Kusini, Mi Casa Music watatua tena Dar es Salaam. Hii itakuwa ni awamu yao ya pili kuja Tanzania.



Hits kama Jika na La Vida zitapigwa live. Wale walioshuhudia show yao ya kwanza, wanajua moto wa jamaa hawa.

Funga kazi, ni November 23, pale ambapo kundi la muziki linalotafutwa zaidi kwa show barani Afrika, P-Square litakuja kuitikiza Dar es Salaam.



Alingo na Personally zitapigwa live na Peter na Paul Okoye. Ama kweli patachimba.


Dar Mpo tayari Kuparty....?
Previous Post Next Post