Ni takriban miaka miwili sasa imepita baada ya muimbaji wa muziki wa injili nchini Rose Muhando kusaini ‘record deal’ na kampuni ya Sony Music Africa. Mkataba huo ulisainiwa February mwaka jana jijini Dar es Salaam.
Rose Muhando (Katikati) akiwa na wawakilishi wa Sony Music Africa akiwemo Seven Mosha (kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa hafla ya kusaini mkataba huo February mwaka jana
Mkurugenzi na Mkuu wa Vipaji na Biashara Mpya Afrika wa Rockstar 4000 / Sony Music Africa, Seven Mosha, amesema exclusively kuwa mwishoni mwa mwaka huu kazi mpya za Rose Muhando zitaanza kutoka. Amesema kwa kipindi chote hicho, Rose Muhando alikuwa akirekodi nyimbo mpya kwenye studio za Sony Music Afrika zilizopo nchini Afrika Kusini.
“Ni utaratibu tu wa kawaida, kutengeneza nyimbo ambazo zina hadhi ya kiasi fulani, kutengeneza music videos na kumweka kwenye training kadhaa ya vitu tofauti,” Seven amesema kueleza sababu za kazi mpya za Rose Muhando kutoanza kusikika hadi sasa.
AY, Ali Kiba, Rose Muhando, Diamond na Mwana FA
Seven amesema nyimbo za Rose akiwa chini ya label hiyo zitaendelea kuwa zile zile zilizoeleka KWA watu wengi lakini kilichobadilika tu ni ubora wa utayarishaji.
“Producers ambao alifanya nao kazi ndio hao hao, ni studio tu zilizotumika South Africa. Kwahiyo timu yake nzima ya production tulienda nayo South Africa,” amesema.
Akielezea tofauti aliyonayo msanii huyo kwa sasa, Seven amesema kipaji chake kiko pale pale na wamekiboresha zaidi kuwa na hadhi ya kimataifa na uwezo wa kuitumia sauti yake vizuri zaidi.
“Kama collaborations tofauti tofauti, sauti yake kusikika vizuri zaidi. Kwahiyo ni personal growth ya msanii ambayo utaskia tofauti.”
Seven ameongeza kuwa mafunzo aliyoyapitia Muhando ambaye kwa sasa yupo kwake mjini Dodoma ni pamoja na uhusiano wa umma, bima na masuala ya fedha.
Tags:
celebrity News