Rashid Matumla adai mdogo wake Mkwanda ameitia aibu familia kwa kukamatwa na unga


Bondia wa zamani, Rashid Matumla amesema iwapo ikithitika kuwa mdogo wake, Mkwanda ni kweli anajihusisha kusafirisha dawa za kulevya, atakuwa ameipa aibu kubwa familia yao.


Rashid Matumla

Akihojiwa jana na gazeti la Mwananchi, Rashid aka Snake Boy amesema kitendo hicho kinaitia aibu familia yao hasa kwakuwa ni haramu sit u Tanzania tu bali na kwenye nchi zingine pia.

Mkwanda alikamatwa wiki iliyopita nchini Ethiopia akiwa na mchezaji wa zamani wa Simba, Joseph Kaniki na leo watapandishwa kizimbani nchini humo kwa tuhuma hiyo.

“Mimi mwenyewe nashangaa ni lini amejiingiza kwenye kazi hiyo, hata wakati anaondoka hakuniaga, mimi kaka yao na familia hatuelewi chochote,” alisema Matumla.

Aliongeza kuwa mdogo wake huyo alikuwa amebadilisha uraia na kuchukua uraia wa Sweden na kuoa hukohuko Sweden licha ya kwamba hapa Tanzania alikuwa amepanga Mbagala, Dar es Salaam na alikuwa anakuja na kukaa kwa muda na kisha kuondoka.

“Ni mwezi sasa umepita sina taarifa naye na hata wakati anaondoka hakuniaga, nimesikia kupitia vyombo vya habari kitendo cha mdogo wangu kukamatwa kimenisikitisha mno, siyo siri nimekwazika na ninarudia kusema hii ni fedheha kwenye familia yetu,” alisema Rashid.

Source: Mwananchi
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA