Picha: H. Baba na Flora Mvungi wapata mtoto wa kike ‘Tanzanite’



Ni Furaha kubwa kwa Ndoa ya msanii wa bongo fleva Hamis Ramadhan aka H.Baba na mkewe Flora Mvungi imefanikiwa kupata mtoto wa kike waliyempa jina la ‘TANZANITE’.


Tanzanite

Mke wa H.Baba  "Flora" amejifungua salama jana (September 11) majira ya saa 12.30 jioni katika hospitali ya Marie Stopes iliyopo Mwenge.



“Najiskia furaha sana kwasababu hii ndiyo mara ya kwanza naitwa baba, namshkuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunipa mtoto wa Kike ambaye tumemuita Tanzanite Hamis, nawashukuru wote pia ambao wametuombea dua” Alisema H.Baba

Timu Nzima ya Bongo 61 inapenda kuwapa hongera H-Baba na Flora kwa kupata mtoto mzuri na mwenye afya.... 
Previous Post Next Post