Zaidi ya Shilingi milioni 50 zamtoka Diamond kushoot video ya wimbo wake mpya ‘Namba 1′



Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz ametumia dola 30,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 50 na zaidi za Kitanzania kushoot video ya wimbo wake mpya, Namba Moja nchini Afrika Kusini.

Akiongea na gazeti la Mtanzania, Diamond amesema wimbo huo utasikika hewani katika vituo mbalimbali vya redio siku za hivi karibuni.
“Siku zote mimi ni muumini wa vitu vizuri ,nimegharamia wimbo wangu sasa nakuja kuwashika tena mashabiki wangu kwa Namba Moja, hii ngoma nimerekodi Afrika kusini,”alisema Diamond.
Previous Post Next Post

Popular Items