Skendo ya Rose Ndauka, Mapya yaanza kuibuka, eti ni ishu ya kutengenezwa.



Hivi majuzi kuliibuka skendo ya kuvunja amri ya sita iliyomkabili mwanadada Rose Ndauka na mwanamuziki wa bongo fleva anayechipukia Nassoro Ayoub “Nasry” au Tajiri Boy kuwa wawili hawa wamekutwa kaitka hoteli moja jijini Dar es Salaam wakivunja amri ya sita ilhali ni mwezi mtukufu wa Ramadhani na pia ikifahamika kwa jamii kuwa Rose Ndauka amechumbiwa na mchumba wake Malik ambaye wanatarajiwa kuoana hapo baadae.
Katika sakata hilo lililoripotiwa na vyombo mbalimbali vya kuanzia gazeti moja maarufu la udaku nchini zinasema wawili hao waliingia hotelini hapo na kutoka masaa kadhaa baadaye huku Rose ndauka akiwa amejifunika na hijabu ili asionekane na mpenzi wake huyo mpya lakini kwa bahati mbaya “wadau”walimpiga picha na kusambaza habari hiyo.


Hapo jana mtandao wa filamu central uliripoti kutokana na uchunguzi wao kuwa tukio hili lote ni picha ya kutengenezwa ili kumtoa kisanii mwanamuziki Nassoro Ayoub “Nasry” anayetaka kupata umaarufu katika upande wa bongo fleva kwa njia hiyo ya skendo ili wananchi wamfahamu
Mtandao huo umeripoti zaidi kuwa mchezo huo wote umafanikiwa baada ya Rose Ndauka kukubali “kutumika” kwa kupewa kitika cha milioni moja ili afanye mambo hayo.
Habari hiyo inasema zaidi kuwa hapo mwanzo walimfuata mwanadada Jacqueline wolper ili afanye mchezo huo lakini akagoma kwa kuhofia kupoteza heshima yake na ndipo alipofuatwa Rose ndauka na kukubali.
Bado tunaendelea kutafuta taarifa zaidi ili tuweze kupata ukweli halisi wa tukio hili.

Tunaomba Utupe maoni yako! 
Previous Post Next Post