Ronaldo ataka mshahara Pauni 320,000



ronadlo f2253

CRISTIANO Ronaldo ameikaba koo Real Madrid. Anafahamu wazi, rekodi yake ya uhamisho wa Pauni 80 milioni inayoshikilia dunia kwa sasa itavunjwa na Gareth Bale na hivyo sasa ametafuta namna ya kuendelea kuwa na hadhi kubwa katika klabu hiyo.
Supastaa huyo wa Ureno, amesema atakubali kuendelea kubaki Santiago Bernabeu na kucheza sambamba na Bale kama tu atalipwa mshahara wa Pauni 320,000 kwa wiki.


Ronaldo bado anataka kubaki nchini Hispania, licha ya kuhusishwa na mpango wa kujiunga na Manchester United na Paris Saint-Germain.
Akitambua rekodi yake itavunja, Ronaldo sasa ametaka kulipwa mara mbili ya mshahara atakaolipwa Bale ili aendelee kuwa namba moja kwa wachezaji wenye hadhi kubwa katika klabu hiyo ya Hispania.
Sambamba na hilo, Ronaldo anatarajia klabu yake kumpigia kampeni za nguvu katika mchakato wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Dunia na anataka pia kupatia fursa za kibiashara atakazofungua Asia na Amerika.
Baada ya kufunga mabao 175 katika mechi 167 alizochezea Real Madrid, Ronaldo anataka mshahara wake upande kwa kasi, licha ya mkataba wake kubakiza miaka miwili.
Suala hilo sasa linatarajiwa kuwafanya mabosi wake waanze kukuna kichwa kuhusiana na namna ya kutekeleza matakwa yake ili kumkutanisha na Bale kikosini:
Previous Post Next Post

Popular Items