MAN CITY YAMSAJILI STEVAN JOVETIC



city2 c3ad6
 Mshambuliaji Stevan Jovetic ametambulishwa Man City (HM)
 city 6879c
Mshambuliaji, Stevan Jovetic
KLABU ya Manchester City imethibitisha kumsaini mshambuliaji Stevan Jovetic kutoka Fiorentina kwa ada ya Pauni Milioni 25.8 baada ya mwanasoka huyo wa kimataifa wa Montenegro kufuzu vipimo vya afya uwanja wa Etihad. 

Inafahamika City watalipa kiasi cha Pauni Milioni 22.4 na ada itapanda kutokana na kukuwa kwa malipo ya posho.

Uhamisho wa Alvaro Negredo pia umethibitishwa, huku yeye akipewa jezi namba tisa. 

Chanzo: Sportmai
Previous Post Next Post

Popular Items