Octopizzo wa Kenya kupanda jukwaa moja na rapper wa Marekani 2 Chainz huko Uingereza



Yule Hit maker wa ‘Ivo Ivo’ Octopizzo anazidi kudhihirisha ukomavu wake katika cheo chake kipya cha ‘ustaa’ baada ya kuchaguliwa kuiwakilisha Kenya katika ‘UN-Convention Conference’, mkutano unaotegemewa kufanyika (September) mwaka huu huko Birmingham,Uingereza.
Octopizzo_Octopizzo
Octopizzo ambaye alitoa habari hiyo kupitia ukurasa wake wa facebook, anategemewa kupanda jukwaa moja na rapper wa Marekani 2 Chainz ambaye pia yuko katika orodha ya wasanii 33 wa kimataifa watakao perform.
chainz
2 Chainz
Rapper huyo wa Kibera Namba Nane Octopizzo ndiye msanii pekee wa Kenya aliyechaguliwa kuwakilisha nchi hiyo kati ya wasanii 33 wa kimataifa waliochaguliwa kuperform katika mkutano huo wenye lengo la kujenga uelewa juu ya mapambano ya vita na migogoro.
Previous Post Next Post