Mabeste atarajia kuitwa baba siku yoyote kuanzia leo



Kukiwa kuna muendelezo wa wasanii wa muziki wa kizazi kipya kupata watoto leo msanii wa muziki huo Mabeste amesema naye anatarajia kupata mtoto muda wowote. Amesema mtoto huyo akiwa wa kiume atampa jina, Kendrick na kama akiwa wa kike atamuita Kelly.
306540_332593690173224_2037399722_n
Muda mchache uliopita Mabeste alikuwa maeneo ya Mikocheni akifanya manunuzi ya maandalizi ya kijacho, ambapo amesema alikuwa ananunua mapambo ya chumba cha mwanae huyo pamoja na stika kwaajili ya kuta za chumba atakapokuwa akilala mtoto.
“Kupata mtoto kwetu ni neema kwani nilikaa kwa muda mrefu bila kuongea na baba yangu lakini baada ya kinachokaribia kuja mabadiliko yametokea ndio maana tumechagua majina yenye maana kwaajili ya kijacho,”Mabeste ameongea na kipindi cha XXL .
Previous Post Next Post