Unaweza kuamini kuwa kuna champagne inauzwa dola milioni 1.8 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 2.9 za Tanzania? Huwezi kuipata champagne iitwayo Goût de Diamants bila mkwanja huo.
Wakati bado unaendelea kuwaza kiwango hicho cha fedha, basi mwanamuziki kipenzi cha warembo wa Nigeria, Wizkid ambaye wiki hii alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa, ameburudika la kinywaji hicho ambacho ni cha ghali zaidi kuliko champagne zote duniani.
Liam na Wizkid wakiwa na chupa ya Goût de Diamants (champagne ghali zaidi duniani)
Alexander Amosu: Jamaa aliyeitengeneza chupa ya champagne hiyo alipost picha ya Wizkid na Liam (mwanamuziki wa kundi la One Direction la Uingereza inayomuonesha Wizzy akinywa champagne hiyo kwenye sherehe aliyoifanyia jijini London.