PICHA ZA STEREO BAR KINONDONI BAADA YAKUTEKETEA KWA MOTO JIONI YA JANA.


Haya Mabaki ya Stereo Bar


 Moto ukiendela kuteketeza Stereo Bar huku umati wa watu ukiangalia
Moshi ulikuwa mweusi sana ni maajabu ya Mungu kwamba wote waliokuwa humo walitoka salama. 


 Moto ulikuwa mkubwa sana na ulitambaa kwa kasi kubwa sana. Mungu mkubwa hakuna mtu aliye umia. Na pia inasemekana kulikuwa na maandalizi ya kitchen party au send off ya mdada ambayo ilikuwa ifanyike jioni hiyo na huko ukumbini ndiko moto huo ulipo anzia.
Watu wakiendelea kushangaa
Wakuokota makopo na vitu bila kuogopa atahri za moto pia walikuwepo maana bado mbao zenye moto zilikuwa zinadondoka toka juu
Ndani ya Stereo kila kitu nyanga' nyanga'
'Java' imebakia jina tu
Huu ni ukuta wa nyumba ya jirani ambyao nayo iliunguwa na mali nyingi sana kuharibika. Kama mnavyo ona simtank lote limeyeyuka. Huko ndani ndo usisemee. Wenye nyumba walipanic sana ilikuwa kama msiba pale na hawakupenda picha zozote za nyumba yao kuchukiliwa.
Bar maarufu Kinondoni iitwayo 'STEREO' imateketea kwa moto mkubwa sana jioni ya jana. Moto huo unadhaniwa ulitokana hitilafu ya umeme katika bar hiyo. Pamoja na bar hiyo kuteketea pia nyumba tatu  lilizokuwa jirani na bar hiyo pia zimeathirika na mali nyingi kuharibika. Inasemekana hii ni mara ya pili Bar hii kuungua japo mara yakwanza waliuwahi moto.
Previous Post Next Post

Popular Items