Kanye West akanusha taarifa za Kuwa yeye kumcheat mama kijacho wake Kim Kardashian na mrembo mwingine!



Wakati couple ya rapper Kanye West na Kim Kardashian ina count down siku za mtoto wao wa kwanza kuja duniani, wameendelea kuandamwa na scandal zenye dalili za kuivuruga familia hiyo.
Kanye West akiwa na binti huyo iatwaye Leyla
Wiki hii model aitwaye Leyla Ghobadi mwenye miaka 24 aliliambia jarida la ‘US Magazine Star’ kuwa amekuwa na mahusiano ya kimapenzi na rapper huyo kwa muda sasa . Leyla amedai alikutana na Kanye mwaka jana (2012) katika moja ya show zake ambayo na Kim alihudhuria pia, ambapo walinzi wa Kanye walimchomoa katikati ya umati wa watu na baadae walienda out yaani yeye na Kanye.
Msichana huyo wa mwenye asili ya Canada aliendelea kusema baada ya hapo walikuja kushiriki tendo la kumtengeneza mtoto pamoja (of course kwao halikuzaa tunda) katika hotel ya Atlantic City wakati mpenzi wa Kanye Kim Kardashian alikuwa tayari ni mja mzito.
Leyla ghobadi
Hizo zilikuwa ni tuhuma za mlalamikaji, upande wa mtuhumiwa, Kanye kupitia mwakilishi wake ameuambia mtandao wa TMZ kuwa tuhuma hizo si za kweli hajamcheat Kim na hayo ni mashambulizi tu ya wabaya wanotafuta umaarufu na kuivuruga familia yao hasa kipindi hiki wanapokaribia kupata mtoto. “It’s a blatant attempt by a misguided individual who is clearly seeking publicity, and another in a series of malicious stories drummed up by non-credible ‘news’ sources.” Alisema.
Msemaji huyo aliongeza “This is a sad attempt to hurt two people trying to live their lives.”
Model huyo ambaye ni sister from another mother wa Drake (sababu wote ni wa Canada) alimalizia kwa kusema Kanye alimtafuta wikendi iliyopita akitaka waonane kwaajili ya ‘game’ ya mara ya 3! really Kanye?
Previous Post Next Post

Popular Items