Uteuzi huo umefanywa na kampuni ya Nollywood Entertainment Ltd UK ambao ni waandaji wa tuzo hizo.
Kazi ya Sporah itakuwa ni kukusanya na kupokea filamu kutoka nchi za Afrika Mashariki na pia kualika viongozi wa serikali wa nchi hizo na balozi ili kushuhudia tuzo hizo zitakazofanyika kwa siku tatu.
Siku hizo ni pamoja na siku 2 za semina ya filamu, maonesho ya utamaduni, jukwaa la uwekezaji na usiku wa tuzo zenyewe. Mwaka huu ZAFAA zitaanza tarehe 14 November hadi tarehe 16.
Tunampa pongezi Sporah kwa uteuzi huo.