SHOW ZA LADGY GAGA & KANYE WEST ZITAONEKANA KWENYE SMARTPHONES


KANYE WEST & LADY GAGA
Nyota wa Kimataifa, Kanye West pamoja na Lady Gaga wapo katika mpango mkubwa kabisa wa kuwa wanarusha maonyesho yao Live kupitia smartphones kwaajili ya asilimia kubwa ya mashabiki wao ambao huwa wanakosa kuhudhuria maonyesho haya moja kwa moja.
Huduma hii itaanza kufanya kazi hivi karibuni ambapo huduma hii itakuwa haimruhusu mtu kurekodi videos za maonyesho haya na kusambaza kwa wengine na mtumiaji ataweza kuona dakika chache za kwanza za tamasha lenyewe bure kabla ya kuanza kulipia.
Mbali Lady Gaga pamoja na Kanye West, Msanii mwingine ambaye amekubali kuingizwa katika mpango huu ni John Legend na zoezi hili litaanza hivi karibuni.
Previous Post Next Post