KUMBE CONRAD ALIKUWA MCHOVU



conrad
Siku moja tu tangu kuanza kwa kesi mpya ya kifo cha Michel Jackson, imefahamika kuwa, aliyekuwa daktari wa MJ, Conrad Murray alikuwa katika wakati mgumu sana kifedha wakati alipopata shavu la ajira kama mwangalizi wa Afya ya Michael.
Hii ni kutokana na maelezo ya ushahidi wa polisi mmoja katika kesi hiyo kuwa Murray ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka minne kutokana na kifo cha Michael Jackson, alikuwa na madeni makubwa ikiwepo ada za watoto, bili mbalimbali pamoja na kodi za biashara yake.
Gonga continue rading kuendelea..
Hii ni katika hatua ya wanasheria wa upande wa madai kuthibitisha ushahidi kuwa, Daktari huyu alikuwa katika matatizo makubwa kipesa, na alikuwa tayari kufanya lolote hata kuvunja miiko ya taaluma yake ili kujipatia pesa.

Kesi hii imefunguliwa na Katherine Jackson, mama wa Michael ambaye ana madai dhidi ya kampuni ya AEG Live ambayo ilikuwa inaandaa tamasha la mwisho la Michael kwa kutojali afya ya msanii huyu na kupelekea kifo chake.
Previous Post Next Post

Popular Items