David Beckham na Zlatan Ibrahimovic wakishangilia kuiwezesha PSG kutwaa taji la kwanza baada ya miaka 19.
Beckham akipongezana na Carlo Ancelotti, kocha wa PSG
Ibrahimovic
Beckham akikumbatiana na mmiliki wa Qatari TV, chaneli ya Al Jazeera Sport ambaye pia ni mmiliki wa PSG, Nasser Al-Khelaif
KIUNGO wa David Beckham ameweka rekodi ya kutwaa mataji ya Ligi Kuu na klabu za nchi nne tofauti, baada ya PSG kuifunga Lyon 1-0 na kutwaa ubingwa wa Ligue 1, Ufaransa.
Beckham, ambaye sasa anakuwa mchezaji wa kwanza wa England kutwaa mataji katika nchi nne tofauti, aliingia akitokea benchi, wakati Jeremy Menez alipokifungia bao pekee la ushindi kikosi cha Carlo Ancelotti.
Ubingwa wa PSG hautathibitishwa hadi Kamati ya Nidhamu ya Ligi itakapokutana kuamua kuipokonya pointi au la kufuatia tuhuma za Mkurugenzi wake, Leonardo kumrubuni refa.