li
Mchezo ulisimama kwa muda sababu ya ubaguzi
Balotelli
Balotelli na Kevin Prince-Boateng wakiwa wamesimama pamoja wakati wa tangazo linatolewa uwanjani
Sulley Muntari alitolewa nje kwa kumsihi refa
MECHI ya AC Milan ya Serie A usikuwa jana ilisimama kwa muda kwa sababu kejeli za kibaguzi ambazo zilielekezwa kwa Mario Balotelli na wachezaji wengine weusi kutoka kwa mashabiki wa Roma.
Refa Gianluca Rocchi alisimamisha mechi na mtangazaji wa uwanjani akawaambia mashabiki wa Roma waache kuwafanyia ishara za nyani wachezaji weusi wa Milan, vinginevyo mechi itaahirishwa.
Mapema Sulley Muntari alitolewa nje kwa kadi nyekundu wakati anakwenda kumsihi refa huyo aliyeonekana aataka kumpa kadi ya pili ya njano Balotelli.
Massimo Ambrosini alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokwenda kulalamika kwa refa Rocchi kabla ya mechi kusimamishwa.
Totti baadaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu beki wa Milan, Phillipe Mexes na mechi hiyo ikaisha kwa sare ya bila kufungana.
Mchezo wa kirafiki Januari baina ya Milan na Pro Patria ulisimamishwa pia kwa sababu kejeli za kibaguzi alizofanyiwa Kevin-Prince Boateng.
Shirikisho la soka Italia limeweka sheria mpya kuwasaidia marefa kudhibiti ubaguzi baada ya kiungo wa Milan, Kevin-Prince Boateng kuamua kuondoka uwanjani January katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Pro Patria baada ya kukutana na dhalili hiyo.