NAMELESS NA WAHU WATARAJIA KUPATA MTOTO WA PILI




Wahu na Nameless wanategemea kupata mtoto wa piliCouple ya mastaa kutoka Kenya, Wahu na Nameless inategemea kuungana na couples za mastaa wengine duniani kama Kim Kardashian na Kanye West, kupokea ujio wa member mpya katika familia zao kutokana na Wahu kuwa mjamzito wa mtoto wa pili.




Baada ya kuwepo uvumi kuwa Wahu ni mjauzito wa mtoto wao wa pili, hitmaker huyo wa ‘Sweet love’ amethibitisha kuwa kweli na anategemea kujifungua mapema mwezi August mwaka huu. Kupitia ukurasa wake wa facebook Wahu alimjibu fan mmoja ambaye ni miongoni mwa fans wengi waliokuwa wakitaka ukweli kuhusu uvumi huo ambao ulithibitishwa kwa jibu lake fupi, “Yes I am”.

Akiwa na excitement ya mtoto wa pili Wahu pia anategemea kuachia single mpya mwishoni mwa wiki hii, wimbo ambao Wahu aliuambia mtandao wa standard media wa Kenya kuwa itakuwa ni hit song kama ilivyokuwa “Sweet Love” na “Running Low”.

Mtoto wa kwanza wa Nameless na Wahu aitwaye Tumiso Nyakwea alizaliwa mwaka 2006 na wimbo wa “Sweet Love” ulikuwa ni dedication kutoka kwa mama yake, na ni wimbo ambao umemletea matunda ya tuzo kadhaa.

Wanamuziki na wanandoa hao, walifunga ndoa 2005, ambayo imefanikiwa kutoa majibu ya mtoto wa kike anayetegemea kupata mdogo wake hivi karibuni.
Previous Post Next Post