KIM KARDASHIAN NA KANYE WEST WAFAHAMU JINSIA YA MTOTO WAO!




Ikiwa ni wiki chache zimebaki kabla ya miezi 9 ya ujauzito wa mpenzi wa Kanye West, Kim Kardashian kutimia, hatimaye jinsia ya mtoto mtarajiwa wa wapenzi hao mastaa imefahamika.


Jana (May 23) ilikuwa ni siku muhimu kwa wazazi watarajiwa Kim kardashian na Kanye West kukutana na daktari kwaajili ya kupigwa ultrasound kujua maendeleo ya kiumbe cha Kanye kilichoko ndani ya tumbo la Kim, pia kuweza kufahamu jinsia ya mtoto wao mtarajiwa.

Kutokana na umuhimu wa appointment ya kujua jinsia ya mtoto mara nyingi wazazi wote wawili huwa wanakwenda pamoja lakini Kanye hakuweza kuungana na kipenzi chake kumuona daktari kutokana na kuwa na ratiba ngumu, japo aliwahi kumwambia mpenzi wake huyo kuwa hatapenda kushiriki katika reality show yao ya ‘The Kardashian’s’, ambayo ilikuwa ikirekodiwa wakiwa hapo kwa daktari. Kim K alisindikizwa na wanafamilia wake wakiongozwa na mama yake mzazi pamoja na dada zake wawili.


Baada ya Ultra Sound daktari alimwambia Kim K jinsia ya mwanae lakini sehemu hiyo ilikatwa katika video clip ya reality show hiyo, hali ambayo imefanya baadhi ya watu kuamini kuwa Kim na Kanye wamependa jinsia ya mtoto wa iwe surprise kwa wengine japo habari za chini ya kapeti zinasema wanatarajia kupata mtoto wa kike.


Kuashiria siku ya kujifungua imekaribia Kim K anategemea kufanya baby shower June 2 na kadi za mwaliko zimeshaanza kusambazwa. Mhariri wa Bongo5 yuko busy kufuatilia uwezekano wa kuhudhuria baby shower hiyo, just kidding!!
Previous Post Next Post