MTOTO WA KIKE WA NATORIOUS B.I.G AMUENZI BABA YAKE KWA KUANZISHA CLOTHING LINE INAYOBEBA JINA LA BABA YAKE "NATORIOUS"




May 21 ilikuwa ni birthday ya rapper marehemu Notorious B.I.G a.k.a Biggie Smalls na Siku iliyofuata mtoto wake wa kike aitwaye T’yanna Wallace mwenye miaka 19 ametambulisha clothing line yake ambayo imebeba jina la baba yake ‘Notorious’.


Notoriouss Clothing line itakuwa ikijihusisha na utengenezaji wa T-shirts pamoja na vitu vingine vya fashion. Moja ya designs za T-shirts zilizotoka ina nembo kubwa ya ‘Notorious’ kifuani na chini yake kuna picha ya bunduki mbili ambazo ni kama ishara ya jinsi baba yake alivyouwawa kwa kupigwa risasi March 9, 1997.


Marehemu Notorious B.I.G aliacha watoto wawili ambao ni wa kiume Christopher Jordan Wallace a.k.a CJ pamoja na wa kike ambaye ni T’yanna.
Previous Post Next Post

Popular Items