Ili kupata likes nyingi kwenye mitandao ya kijamii ni lazima uwe na kitu cha kuvutia. Sio kila mtu ana bahati ya kuwa na maelfu ya likes na followers kwenye Facebook na Twitter. Kwa mujibu wa takwimu za sasa, watangazaji wa Clouds FM ndio wanaongoza kwa kuwa na followers wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii.
Licha ya kuwa mtangazaji wa radio Tanzania mwenye likes nyingi zaidi Facebook, jana mtangazaji huyo wa kipindi cha Amplifaya amekuwa celeb wa pili nchini kufikisha likes zaidi ya laki moja baada ya Masanja Mkandamizaji.
Mpaka sasa Millard ambaye ni mtu wa tatu kwenye orodha ya mastaa 20 wenye ushawishi nchini (kwa mujibu wa Bongo5), ana zaidi ya followers 44,513 kwenye Twitter.
Kilichomponza mtangazaji huyu maarufu kwa kuchombeza kwenye kipindi cha XXL, ni kuwa mpaka sasa anatumia akaunti ya kawaida ya Facebook ambayo ina kikomo cha watu 5,000 tu. Lakini kwakuwa Facebook waliongeza option ya ‘subscribe’ kwenye akaunti ya aina hii, Adam amevutia subscriber 24,036 mpaka sasa. Angekuwa mbali kama angefungua akaunti za watu mashuhuri kama wenzie. Kingine Adam sio maarufu sana kwenye Twitter kama wenzie kwakuwa mpaka sasa ana followers 8,948 tu.
1. Millard Ayo
Licha ya kuwa mtangazaji wa radio Tanzania mwenye likes nyingi zaidi Facebook, jana mtangazaji huyo wa kipindi cha Amplifaya amekuwa celeb wa pili nchini kufikisha likes zaidi ya laki moja baada ya Masanja Mkandamizaji.
Mpaka sasa Millard ambaye ni mtu wa tatu kwenye orodha ya mastaa 20 wenye ushawishi nchini (kwa mujibu wa Bongo5), ana zaidi ya followers 44,513 kwenye Twitter.
2. Dj Fetty
Mpaka sasa Dj Fetty ana likes 61,645+ kwenye mtandao wa Facebook na followers 29,552+ kwenye Twitter.
3. Diva Loveness Love
Mpaka sasa mtangazaji huyu wa kipindi cha Ala za Roho ana likes 33,469+ na followers 29,701 kwenye Twitter.
4. B12
Ni wazi bila sauti ya B12, XXL hupwaya. Mpaka sasa mtangazaji huyu maarufu kwenye utengenezaji wa matangazo ya burudani nchini ana likes 33,813+ na followers 17,176 kwenye Twitter.
5. Adam Mchomvu
Watangazaji wengine nje ya Clouds FM walio na followers wengi kwenye mitandao hiyo ni pamoja na Salama Jabir mwenye likes 21,343+ Facebook na 30,711+ kwenye Twitter. Vanessa Mdee wa Choice FM ana followers 19,897 kwenye Twitter huku Jokate Mwegelo wa Channel O akiwa na likes 18,666+ Facebook na followers 31,861 kwenye Twitter.