KILA MTU KUISHABIKIA YANGA NA KIPENDA YANGA




Mwenyekiti siku ya leo umenikwepa sana hata simu zangu umekuwa haupokei mwanzo nilidhani tatizo la network , ila sasa nimejua tatizo pole sana.

Binafsi nasema ukweli na si ushabiki timu yenu inahitaji mabadiliko hasa sehemu ya ulinzi bado mna tatizo kubwa kwenye defence bila ubora wa kipa wenu ambaye sasa anakuwa Tanzania 2 baada ya kipa ambaye alikuwa anamuweka benchi Simba , Ali Mustapha leo mbele ya kocha mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemuonyesha kuwa anafaaa kukaa langoni mechi inayofuata ya Taifa stars katika kuwania kufuzu Kwa kombe la dunia Hapa nani anabisha Ali Mustapha ana uwezo sasa kuzidi Kaseja?

Najua Soka la Bongo bila Yanga na Simba halitanoga hivyo siwezi omba mabaya kwa simba nawaomba uongozi wa simba pamoja na benchi la ufundi mjipange kwa msimu ujao, na Ndugu zangu yanga mimi nimefurahi leo ila kesho mtanifanya niwe sina furaha tena maana nadhani kwenye klabu bingwa kama tutatolewa raund ya Kwanza hivi!...

Yanga msibweteke Viva Yanga fanyeni kweli mpaka mmchukue ubingwa wa Klabu Bingwa hapo sijui Maggid Mjengwa atajificha wapi? ha ha ha ha leo Simba mngeshinda aisee Mwenyekiti ungeongea sana maana ushindi kwenu ulikuwa ni kwaajili ya kuwaponda Yanga haukuwa na manufaa maana hata Kombe la shirikisho hamna nafasi.
Previous Post Next Post