SILIMA AFUNGUA DUTY FREE SHOP YA KISASA, DODOMA




Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Supermarket (Duty Free Shop) ya pili ya Jeshi la Magereza iliyojengwa katika Mkoa wa Dodoma




Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima kufungua Supermarket (Duty Free Shop) ya pili ya kisasa ambayo imejengwa na jeshi hilo, katika Gereza Isanga, mjini Dodoma. Ufunguzi huo umefanyika leo mjini humo.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akizungumza na maafisa magereza kabla ya kufungua Supermarket (Duty Free Shop) ya pili ya kisasa ya Jeshi la Magereza ambayo itawawezesha maafisa wa jeshi hilo, askari na familia zao kupata huduma ya kununua bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, John Minja na kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Military Shops ambaye ndiye aliyewekeza katika Supermarket hiyo, Afzal Meghji.
Previous Post Next Post